Aangua kilio kushindwa kwa kura 67

30Oct 2020
Ibrahim Joseph
Dodoma
Nipashe
Aangua kilio kushindwa kwa kura 67

​​​​​​​MGOMBEA udiwani Kata ya Nzuguni kupitia CHADEMA, Godfrey Chipungu, amejikuta akiangua kilio mbele ya wapigakura akiwa haamini matokeo ya uchaguzi huo kutangazwa kuwa mgombea wa CCM ameshinda.

Aliyekuwa mgombea udiwani Kata ya Nzuguni, jijini Dodoma jana, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godfrey Chipungu, akiangua kilio baada ya matokeo kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo, Hamisi Jingwa (hayupo pichani), kuwa ameshindwa. PICHA: IBRAHIM JOSEPH

Kwa mujibu wa karatasi iliyobandikwa na msimamizi wa uchaguzi kata hiyo, Hamisi Jigwa, Chipungu alipata kura 1,958, huku mgombea wa CCM, Aloyce Luhega, akipata kura 2,025.

Baada ya kuona matokeo hayo, Chipungu aliangua kilio mbele ya wananchi waliojitokeza kudai matokeo ambayo walidai kuwa yamechelewa kutangazwa hadi jana asubuhi.

Akieleza sababu za kuangua kilio hicho mbele ya wananchi, Chipungu, alidai kuwa matokeo yaliyobadikwa kwenye vituo yalionyesha kuwa yeye alishinda, hivyo aliamini amehujumiwa.

 

Soma zaidi...https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa