ACT- Wazalendo yaunda kamati ya Ilani Uchaguzi Mkuu 2020

23May 2020
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
ACT- Wazalendo yaunda kamati ya Ilani Uchaguzi Mkuu 2020

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeunda Kamati ya watu nane ya kutayarisha Ilani ya chama hicho kama mojawapo ya maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

majina ya viongozi walichaguliwa katika timu hiyo ya ilani.

Katika taarifa iliyotolewa na Kiongozi Mkuu wa Chama hicho, Zitto Kabwe imesema Ilani hiyo itakuwa yenye majawabu ya changamoto za nchi yetu na maoni ya wananchi yatakayokusanya nchi nzima kwa ajili ya kuandaa rasimu ya Ilani hiyo.

“Timu hii ya Ilani ya ACT -Wazalendo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 itaongozwa na mwanataaluma ndugu Mwanahamisi Singano na Sekretariat yake itakuwa chini ya ndugu Idrisa Kweweta ambaye ni Katibu wetu wa Sera,Utafiti na Mafunzo” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Mbali na Mwenyekiti na Katibu wajumbe katika Kamati hiyo ni Emmanuel Mvula ambaye ni wakili na mtaalamu wa haki za kijamii ,Dkt. Elizabeth Benedict ambaye ni mtaalamu Sekta ya Afya ya chama hicho ,Godluck Mushi mtaalamu Sekta ya Fedha ya chama hicho na Ismail Jussa Ladhu ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu.

Wengine ni Abdul Nondo ,Mwenyekiti Ngome ya Vijana ya chama hicho ,Dkt Janeth Fussi ambaye ni Katibu Ngome ya wanawake ya chama hicho ,Mwanaisha Mndeme ambaye ni Katibu wa Ngome ya Vijana na Edgar Mkosamali ambaye ni Katibu Idara ya Bunge na Baraza la Wawakilishi la chama hicho.

Habari Kubwa