Aga Khan yafanya upasuaji wa kwanza kupunguza matiti

13Aug 2019
Romana Mallya
Dar es Salaam
Nipashe
Aga Khan yafanya upasuaji wa kwanza kupunguza matiti

Madaktari bingwa wa hospitali ya Aga Khan na Muhimbili kwa kushirikiana na wenzao kutoka nchi ya Marekani, Canada na  nchi za Ulaya kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa kupunguza ukubwa wa matiti.

Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam Dk Aidan Njau amesema mpaka sasa mtu mmoja amefanyiwa upasuaji huo huku wengine 150 wamejitokeza kupatiwa huduma hiyo.

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika hospitali ya Aga Khan ambapo upasuaji huo unafanyika amesema timu ya madaktari wa Tanzania wanashirikiaa na mabingwa 11 kutoka nchi hizo.

Pia amezungumzia kuhusu operesheni ya kurekebisha makovu yaliyotokana na ajali mbalimbali zikiwamo za moto kwa wanawake na watoto.

Amesema mpaka sasa waliofanyiwa operesheni za moto tangu Jumapili Agosti 11, 2019 ni 32 na lengo ni kuwafanyia wanawake na watoto 56.

 

Habari Kubwa