Agizo la Rais Magufuli juu ya kuuawa mwanafunzi wa NIT

18Feb 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
Agizo la Rais Magufuli juu ya kuuawa mwanafunzi wa NIT

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kusikitishwa na kifo cha mwanafunzi aliyepigwa risasi na polisi siku ya Februari 16 mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Rais Magufuli ameandika ujumbe wa kusikitishwa kwake na kifo cha Akwilina, na kuagiza vyombo vya dola kuwachukulia hatu waliohusika.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT)....Natoa pole kwa familia,ndugu, wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu......Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili”, ameandika rais Magufuli.

Akwilina alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji jijini Dar es salaam, aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa vurugu za siasa zilizotokea siku ya Ijumaa, akiwa kwenye daladala. 

Habari Kubwa