Ahukumiwa jela miaka mitano kwa kuiba debe la maharage

15May 2022
Na Mwandishi Wetu
Njombe
Nipashe Jumapili
Ahukumiwa jela miaka mitano kwa kuiba debe la maharage

MAHAKAMA ya Mwanzo Lugarawa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imemuhukumu Ombeni Ngwa'vi (25) kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuvunja nyumba ya Evaristo Mgimba na kuiba debe moja la maharage.

Akisomewa shitaka hilo na Mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya Hakimu Timoth Mwakisambwe, imedaiwa kuwa Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Mei 12 mwaka huu majira ya mchana ambapo alivunja nyumba ya Evaristo Mgimba kisha kuiba debe moja la maharage yenye thamani ya shilingi 30,000.

Mtuhumiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo ikiwa ni kinyume na kifungu cha sheria namba 294(1)(a), 258(1) na 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2019.

Habari Kubwa