Ahukumiwa kunyongwa kwa kuua familia yake

13Jul 2020
Neema Hussein
Katavi
Nipashe
Ahukumiwa kunyongwa kwa kuua familia yake

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Sumbawanga imemuhukumu Yustine Robert(35) kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuuwa mkewe pamoja na watoto wake kwa kuwatupa kisimani.

Akisoma shitaka hilo leo July 13,2020 katika Mahakama ya hakimu Mkazi wa Mkoani Katavi, Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo David Mrango, amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha sheria ya kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Jaji Mrango amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo April 5,2013 katika eneo la MajiMoto Wilaya ya Mlele mkoani Katavi kwa kuwatupa kwenye kisima cha maji mke wake na watoto wake wawili.

Jaji huyo amesema ushahidi uliotolewa na mashahidi wa nne wa upande wa mashitaka ulionesha kuwa mtuhumiwa alikuwa na ugomvi wa kifamilia siku moja kabla ya vifo vya wanafamilia wake.

Mrango amesema kuwa mashahidi hao wamesema mtuhumiwa alisikika akisema atafanya tendo la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika eneo hilo.

Jaji Mrango amesema kutokana na ushahidi uliotolewa umemtia hatiani Yustine Robert kunyongwa hadi kufa.

Naye Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Lugano Mwasubila, ameishukuru Mahakama kwa kutenda haki, huku akiitak jamiikuacha kujichukulia sheria mkononi bali wanatakiwa kuacha sheria ichukue mkondo wake.

Habari Kubwa