Aishi juu ya mti kwa siku 7, ashindia matunda na ndizi mbichi

08Feb 2020
Na Mwandishi Wetu
MARA
Nipashe
Aishi juu ya mti kwa siku 7, ashindia matunda na ndizi mbichi

George Mokoro mkazi wa kitongoji cha Genteme kijiji cha Buchanchari wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara ameeleza namna alivyoishi juu ya mti kwa muda wa siku saba ndani ya bonde la mto mara baada ya kuzingirwa na maji akiwa ameenda kuvuna mazao yake shambani.

Mwandishi wa ITV akiwa katika kijiji cha Buchanchari wilaya ya Serengeti mkoani kufuatilia athari za mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha ambazo zimepelekea kaya zaidi ya 400 kupoteza mazao na watu watano kufariki dunia alipata taarifa za kuwepo kwa mtu huyo juu ya mti kwa muda wa siku nane baada ya kuzingirwa na maji akiwa shambani.

Ambapo mazao yake aliyokuwa akitegemea kwa chakula yalisombwa na mafuriko huku familia yake ikisalia bila chakula.

ITV ikafunga safari hadi nyumbani kwa baba huyo mwenye mke mmoja na watoto sita ili kujua nivipi amemudu kuishi porini juu ya mti na maswahibu aliyopata kabla ya kuokolewa na hali aliyonayo kwa sasa baada ya kupoteza chakula chote.

Mke wa Mokoro amedai anaujauzito wa miezi mitatu nakusema hali ya chakula nyumbani ni mbaya na kuiomba serikali uwasaidie.

Hata hivyo Mwenyekiti wa kitongoji cha Genteme Petro Makori na baadhi ya majirani wemeeleza namna walivyopata taarifa na kumuoka mokoro na hali aliyonayo sasa  huku Mwenyekiti akieleza kuwa mbali na mokoro pia kuna wananchi wengine wanne bado wamezingirwa na maji.

CHANZO: ITV

 

Habari Kubwa