Ajali ya bodaboda yaua watatu

06Dec 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Ajali ya bodaboda yaua watatu

 

Na Steven William, MUHEZA

 

WATU watatu wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa Muheza mkoani Tanga, katika ajali ya pikipiki.

 

 

Na Steven William, MUHEZA

 

WATU watatu wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa Muheza mkoani Tanga, katika ajali ya pikipiki.

 

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga, Leopold Fungu, alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea katika eneo la Msangazi barabara ya kutoka Muheza Mjini kwenda Tarafa ya Amani baada ya pikipiki za abiria, maarufu kama bodaboda kugongana.

Fungu aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Yohana Ndede (25) mkazi wa kijiji cha Mkanyageni ambaye alikuwa ni dereva wa pikipiki na Joshua Martine (16) mkazi wa kijiji cha Masimbani ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Muheza.

Habari Kubwa