Ajali yaua wawili Tarime

03Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Tarime
Nipashe Jumapili
Ajali yaua wawili Tarime

WATU wawili wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana eneo la Gamasara wilayani Tarime mkoani Mara.

Akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/ Rorya William Mkonda, amesema ajali hiyo imetokea leo Oktoba 3, 2021 majira saa 3:15 asubuhi na imehusisha basi la Kampuni ya Zakaria na gari aina ya Nissan Safari.

Kamanda huyo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uendeshaji usiozingatia sheria za usalama barabarani hali iliyosababishwa na dereva wa basi.

"Dereva aliamua kupita magari kadhaa barabarani bila kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ndipo akakutana uso kwa uso na gari dogo, ajali hii imesababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali," amesema Kamanda Mkonda.

Hata hivyo, amesema kuwa majina ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo bado hayajapatikana na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.

Habari Kubwa