Ajiua kwa risasi kwa tuhuma za kutaka kumbaka bintiye

02Jul 2020
Dotto Lameck
Ruvuma
Nipashe
Ajiua kwa risasi kwa tuhuma za kutaka kumbaka bintiye

MKAZI wa Kijiji cha Mkako wilayani Mbinga mkoani Ruvuma, Basilius Mwingira amejiua kwa kujipiga risasi baada ya kukabiliwa na tuhuma za jaribio la kutaka kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 10.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Simon Maigwa, amethibitisha kifo cha Mwingiru, huku akisema kuwa marehemu alitumia bunduki aina ya shotgun aliyokuwa akiimiliki kihalali na kwamba kilichompelekea Mwingiru kujiua ni msongo wa mawazo kutokana na tuhuma hizo.

ACP Maigwa amefafanua kuwa marehemu amejipiga risasi jana majira saa moja asubuhi wakati akiwa shambani kwake na mwili wake tayari wameshakabidhiwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi.

Habari Kubwa