Akamatwa na polisi kwa kudanganya upupu dawa ya corona

28Apr 2020
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Akamatwa na polisi kwa kudanganya upupu dawa ya corona

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Ibrahimu Bukuku kwa kusambaza ujumbe WhatsApp kupotosha kuhusu dawa ya corona, ukisomeka, " Dawa ya corona twanga pilipili kichaa sufuria 1 halafu changanya na maji vikombe 5, kunywa kutwa mara 7 kwa siku 3, siku ya 4 chuma upupu kisha jipake".

Ibrahim Peter (26) ambaye Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma akisomea shahada ya Sayansi ya biolojia, anatuhumiwa kuandika na kusambaza ujumbe huo wenye kupotosha jamii kuhusiana na dawa ya corona katika makundi ya WhatsApp kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Miongoni mwa ujumbe alizosambaza ni kwamba ‘Dawa ya #COVID19 inatakiwa utwange pilipili kichaa sufuria moja halafu changanya na maji vikombe vitano na kunywa kutwa mara saba kwa muda wa siku tatu na siku ya nne chuma upupu kisha jipake mwili mzima’.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Simon Maigwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika Kijiji cha Mnyele Wilaya ya Nyasa na kitendo alichofanya ni upotoshaji, taratibu zinakamilishwa ili aweze kufikishwa Mahakamani

Habari Kubwa