Akamatwa na polisi kwa kosa la kumtupa mtoto mchanga chooni

22Oct 2021
Grace Mwakalinga
MBEYA
Nipashe
Akamatwa na polisi kwa kosa la kumtupa mtoto mchanga chooni

JESHI la Polisi mkoani Mbeya, limemkamata Janeth Peter (32), Mkazi wa Kiwira wilayani Rungwe kwa tuhuma za kumtupa mtoto wake mwenye umri wa siku tatu, jinsia ya kike, ambaye baadae alikutwa na wasamaria wema akiwa amefariki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema,  mtuhumiwa huyo amekamatwa Oktoba 20,2021 majira ya saa moja usiku baada ya polisi kufanya msako mkali katika Kata ya Kiwira  na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye amehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo.

Kamanda Matei amesema hadi wanaendelea kumhoji  pamoja na uchunguzi wa kitabibu kwa kushirikiana na wataalam wa afya ili kufahamu endapo alitoa mimba au ana matatizo ya kiafya sambamba na kufahamu sababu ya kufanya tukio hilo la kinyama  na kwamba baada ya upelelezi kukamilika hatua za kisheria zitachukuliwa.

Ikumbukwe kuwa Oktoba 20,2021 majira ya saa tatu asubuhi katika Mtaa wa Makaburini Kata ya Kiwira mwili wa mtoto mchanga ulikutwa ndani ya shimo la choo kilichopo nyumbani kwa Salome Lutengano (36) na ndipo jitihada za kuutoa zilianza lakini tayari alikuwa amefariki dunia.

Habari Kubwa