Magufuli alichowaambia marais wastaafu Mwinyi, Mkapa na JK

11Jul 2020
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
Magufuli alichowaambia marais wastaafu Mwinyi, Mkapa na JK

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana kwa miaka mitano yamefanya na wanachama wa chama hicho pamoja na watungulizi wake.

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho, Rais Magufuli amesema kuwa mpaka sasa bado vijiji elfu tatu tu ambavyo havijafikiwa na umeme nchini. 

"Tunapojenga reli ya kisasa ,hospitali, tunapofufua reli pamoja na kununua meli yote ni mafanikio ya Watanzania " amesema Rais Magufuli 

Mkutano huo ambao unatarajiwa kumpitisha Rais John Magufuli kuwa mgombea wa Chama hicho katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umetanguliwa halmashauri kuu iliyoketi jana na kumpitisha Dr. Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa Urais kwa upande wa Zanzibar.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ,Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana Spika wa bunge mstaafu Anna Makinda na Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustine Mrema.

Habari Kubwa