Aliyemchapa mwanafunzi hadi kufa, ahukumiwa kunyongwa

06Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
BUKOBA
Nipashe
Aliyemchapa mwanafunzi hadi kufa, ahukumiwa kunyongwa

Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba imemhukumu kunyongwa hadi kufa, mwalimu Respicius Mutazangira baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Kibeta, Sperius Eradius mwishoni mwa mwaka 2018.

mwalimu Respicius Mutazangira akiingia mahakamani.

Wakati Respicius akihukumiwa kunyongwa, mwalimu mwenzake ambaye alishtakiwa naye, Heriet Gerald ameachiwa huru.

Hukumu  hiyo imetolewa leo na Jaji Lameck Mlacha ambaye alisikiliza kesi hiyo kwa mwezi mmoja.

 Katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa walimu hao walitenda kosa la kumuadhibu kwa kipigo Sperius kwa madai kuwa aliiba mkoba wa mwalimu Eliet ukiwa na fedha,hata hivyo ilibainika kuwa mkoba huo wa mwalimu herieth ulisahaulika katika pikipiki aliyoipanda mwalimu huyo. 

Mwalimu Heriet Gerald.

Habari Kubwa