Aliyesababisha kushikiliwa ndege ATCL kulipa gharama

04Sep 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Aliyesababisha kushikiliwa ndege ATCL kulipa gharama

Mahakama Kuu ya Gauteng ya nchini Afrika Kusini imeamuru ndege ya Air Tanzania (ATCL) Airbus A220-300 iliyokuwa inashikiliwa nchini humo kuachiwa.

ATCL.

Kufuatia kushikiliwa kwa ndege hiyo kwa zaidi ya wiki moja, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, amesema baada ya kusikilizwa kwa shauri la kesi hiyo leo mahakamani hapo, huku jopo la majaji kutoka Tanzania wakiwemo, mahakama imeamua kuachiwa kwa ndege.

''Mahakama Kuu ya Gauteng, Afrika Kusini, leo imetoa hukumu na kuamuru kuwa ndege ya Air Tanzania, iliyokuwa ikishikiliwa nchini humo iachiwe na mlalamikaji alipe gharama za kesi'', amesema Msemaji.

Aidha Dkt. Hassan Abbas amewashukuru Watanzania kwa kuwa wavumilivu ambapo amesema, ''tunawashukuru wote kwa uvumilivu wenu''. amesema Ndumbaro

Naye Naibu Waziri Mambo ya Nje ya Tanzania, Dk Damas Ndumbaro amesema Serikali ya Tanzania imeshinda kesi hiyo bila kutoa fedha yoyote ambayo aliyetushitaki alitaka Serikali ya Tanzania tuweke fedha kama dhamana dola milioni 33.

“Tumeshinda na ndege imeruhusu kuondoka. Kwa sasa hakuna kesi yoyote.” amesema Ndumbaro

Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ilishikiliwa nchini Afrika ya Kusini Agosti 24,2019, kwa amri ya Mahakama nchini humo, kutokana na kesi iliyofunguliwa na raia mmoja wa huko.

Habari Kubwa