Aliyesomeshwa na Mkapa hadi chuo kikuu afunguka

30Jul 2020
Na Waandishi Wetu
Masasi
Nipashe
Aliyesomeshwa na Mkapa hadi chuo kikuu afunguka

SUNDAY Abdul, mmoja wa wananchi aliyesomeshwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Sanday Abdul, ameeleza alivyoweza kufikia elimu yake kufika chuo kikuu kwa kusomeshwa na Rais Benjamin Mkapa, akilipiwa gharama zote za masomo.

hayati Benjamin Mkapa.

Akizungumza na Nipashe wakati wa Maziko ya kiongozi huyo aliyefariki usiku a kuamkia Julai 24, mwaka huu, alisema walikuwa wanafunzi 12 waliofahulu katika shule msingi Lupaso ambako Mkapa alisoma na kuahidi kuwasomesha hadi atakaposhindwa wao.

“Pamoja na kutulipia ada, lakini alitulipia gharama zote za mahitaji muhimu ya maisha kama chakula, mavazi alitugharamia, na nauli ya kwenda na kurudi kijijini kila shule na vyuo vikufunguliwa na kufungwa, na aliwanunulia vitabu alivyoona vitawasaidia kwenye masomo yao,”alisema.

Abdul alisema alimaliza Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), mwaka 2015 na kupata Shahada ya Ualimu na kwamba kwangu ni baba, kiongozi na mlezi kwa kuwa bila yeyea asingeweza kusoma.

Alikuwa anapenda elimu, aliniambia utasoma hadi pale utakapoacha kusoma, tulimaliza wote hatukumwangusha na wote tunafanya kazi sehemu mbalimbali. Pia kamsomesha mdogo wake.

Alisema alipata taarifa za msiba ikiwa ni siku chache akiwa ametoa kijijini, mdogo wangu aliingia mtandaoni na kunieleza Mzee amefariki nikahakikisha kwa kuingia mtandaoni niliona kwenye vyombo vya habari, nilikuwa Dar es Salaam naelekea Moshi ninapoishi, ikabidi nigeuze nirudi.

Alisema watu walimtegea sana na kwa sasa wanaona mambo mengi yatakwama kwa kuwa alikua na miradi mingi ikiwamo kuanzisha chuo cha Nesi, na kuimba serikali kusaidia miradi hiyo ikamilike.

WANAFUNZI WENZAKE NDANDA

Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekobdari Ndanda, Godfrey Kasawala. ambako Hayati Mkapa alisoma, alisema kupitia umoja wao wamehuzunika kwa kuwa wamepoteza mwanachama na mlezi na kila mwaka huwa wana vikao vya kujadili maendeleo ya kuinua kiwango cha shule hiyo na kiongozi huyo alihudhuria.

“Septemba mwaka jana tulikaa kikao ambacho kilizaa matunda na serikali ilitoa miloni 674 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa majengo mbalimbali.

Tuankumbuka amekarabati na kujenga vziru bweni alililokuwa analala litakuwa ni kituo cha taarifa zake kuanzia historia ya maisha yake, vitabu mbalimbali na nyaraka zitakuwepo kwa ajili ya wanafunzi kusoma,”alisema.

Naye, aliyekuwa Diwani wa Lupaso, Doglaus Mkapa, alisema Mzee Mkapa aliweka ahadi nyingi za kuwafanyia wananchi wa Lupaso, ikiwamo ukarabati wa Shule ya Msingi Lupaso ambayo alisoma (Mkapa), miundombinu ya barabara na ufufuaji wa miundombinu ya maji iliyokufa muda mrefu.

“Nashukuru ukarabati wa shule baada ya kifo serikali imetoa milioni 400 kwa ajili ya ujenzi a shule mpya ya Lupaso, ikiwa ni namna ya kumuenzi Rais Mkapa,”alisema.

Salome Kitomari na Hassan Nasri, Masasi

Habari Kubwa