Anna Mghwira afariki dunia

22Jul 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Anna Mghwira afariki dunia

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia leo Alhamisi Julai 22, 2021 katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mghwira awali alikuwa amelazwa katika hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua na baadaye kuhamishiwa hospitali ya mkoa wa Arusha Mount Meru.

Mghwira aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo, akawa mgombea urais kupitia chama hicho mwaka 2015 na kushika nafasi ya tatu wakati Hayati Dk. John Magufuli aliposhinda uchaguzi huo.

Aliwahi pia kuwa mkuu wa mkoa wa Kiliamanjaro kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 alipostaafu.

Habari Kubwa