Askari Polisi ahukumiwa miaka miwili jela kwa rushwa

21Mar 2019
Godfrey Mushi
MOSHI
Nipashe
Askari Polisi ahukumiwa miaka miwili jela kwa rushwa

Askari Polisi Tufike Tumaini aliyekuwa akikabiliwa mashtaka 13 ya rushwa, amehukumiwa kutumikia adhabu ya miaka miwili jela, baada ya kutiwa hatiani na Mahakama ya Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.

Tumaini ametiwa hatiani kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 600,000.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Wilaya hiyo, Judith Kamala aliieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa ametiwa hatiani baada ya kukiri makosa matano kati ya 13 yanayomkabili.

Askari huyo anadaiwa kutenda makosa hayo kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Namba 11 ya Mwaka 2007.

Katika kesi hiyo namba 27 ya mwaka 2019, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Suzan Kimaro alidai kuwa mshtakiwa alikiri kuwakamata na kuwaweka mahabusu wazazi 10 ili kuwasukuma kutoa rushwa kwa kuhusika katika ucheleweshaji wa usajili wa watoto kujiunga na muhula wa masomo.

Habari Kubwa