Askofu Rwoma akemea vitendo vya kishirikina

23Oct 2020
Lilian Lugakingira
BUKOBA
Nipashe
Askofu Rwoma akemea vitendo vya kishirikina

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Desdelius Rwoma amewataka wakazi wa Mkoa wa Kagera kuacha kujihusisha na vitendo vya kishirikina maana vina hatarisha amani na kusababisha vifo.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Desdelius Rwoma.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa kikao cha kamati ya amani kilichowashirikisha viongozi wa dini, wazee maarufu, waendesha bodaboda na watu wenye ulemavu.

Amesema kuwa kutuhumiana uchawi mbali na kuhatarisha amani, pia kunadumaza maendeleo ya mkoa na nchi kwa ujumla.

Askofu Rwoma amesema kuwa kuna siku aliwahoji baadhi ya waumini wa kanisa hilo wanaotuhumiana uchawi, akitaka waeleze ni kwa namna gani wanalogwa lakini hakuna hata mmoja alikubali kutoa ushahidi juu hilo.

Habari Kubwa