Askofu Shoo awapasha viongozi wenye kiburi

05Apr 2021
WAANDISHI WETU
Dar es Salaam
Nipashe
Askofu Shoo awapasha viongozi wenye kiburi

MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Frederick Shoo, amesema chini ya utawala wa Rais, Samia Suluhu Hassan, wale wote waliokuwa wanajiinua na kujifanya vifutu, wakae mguu sawa, tayari kwa mwendo mbele.

 

Amesema ana imani  hiki ni kipindi cha kuonyesha unyenyekevu na upole, lakini kusimama katika njia ambayo anataka Mungu, na kwamba jambo hilo ni nguvu kubwa sana, kuliko hata nguvu ya wale wanaojiinua na kujifanya vifutu.

 

Askofu Dk. Shoo, alitoa neno hilo jana katika ibada ya kwanza ya ufufuko wa Pasaka, iliyofanyika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi Mjini wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT.

 

Alikuwa akimshukuru Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, baada ya kutoa salaam za serikali katika kanisa hilo.

 

“Mama (Mghwira) nakushukuru kwa kuwa mfano, na mimi nasema chini ya mama Samia Suluhu Hassan, wale vifutu wakae mguu sawa, tayari kwa mwendo mbele.

 

“Sasa Mungu amekupa hekima kubwa, na mimi naona ya kwamba unao uwezo mkubwa, lakini vile vile roho ya unyenyekevu, roho ya upole. Kuna watu wana tafsiri upole kwamba ni udhaifu, unyenyekevu ni udhaifu, sivyo.

 

“Wala maandiko matakatifu hayasemi hivyo, ndiyo maana mimi ni imani yangu kabisa kwamba Mungua taendelea kuwapa nguvu na wewe na wanawake, na sisi wengine kushirikiana na Mheshimiwa Rais (Samia).

Habari Kubwa