Aweso aagiza DDCA kukusanya madeni

28May 2021
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Aweso aagiza DDCA kukusanya madeni

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewaagiza Wakala wa Uchimbaji Visima Nchini (DDCA) kukusanya vyeti (certificate) za madai ya wakandarasi wa uchimbaji visima vya maji, ili ifikapo Juni mwaka huu wawe wameshalipwa madeni yao.

Aidha amewaagiza DDCA, kuhakikisha wanagawa kazi kwa wakandarasi wazawa wenye kukidhi vigezo ili kuhakikisha miradi ya uchimbaji visima inakamilika kwa wakati.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha ya wadau wa maji, kuhusu utafiti na uchimbaji wa visima ya maji nchini, Aweso amesema, ni lazima hivi sasa kwenda na teknolojia ya kisasa, mtu anapofanya kazi lazima alipwe kwa wakati ili kazi ifanyike kwa ufasaha zaidi.

"Malipo ya kazi yanapaswa kuja kwa wakati hakuna sababu ya kuyachelewesha, ndio maana nawaagiza mkusanye certificate za madai yao kutoka kwa wakandarasi ili walipwe na tuanze upya katika kufanya nao kazi ambazo watakuwa wamepewa na wizara.

"Nawaomba ili ninaloagiza lifanyike kwa haraka na muanze kukusanya certificate za hawa,"amesema.         

Habari Kubwa