Aweso amtaka mhandisi mradi wa maji ajitafakari

25Apr 2021
Neema Emmanuel
Mwanza
Nipashe Jumapili
Aweso amtaka mhandisi mradi wa maji ajitafakari

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amemtaka Mhandisi mshauri wa mradi wa tenki la maji la Buswelu unaogharimu billion 6, Andrew Mwakagenda kujitafakari baada ya kumdanganya waziri kuwa wanafanya kazi hadi siku ya Jumapili.

Mhandisi Mshauri mradi tenki la maji Buswelu akkujitafakari kwa uongo

Kauli hiyo ameitoa leo alipotembelea mradi huo na kukukuta hakuna kazi inayofanyika bali Mhandisi hiyo kawaleta wafanyakazi ili kuonyesha wanafanya kazi wakati hakuna shughuli yoyote inayofanyika .

" Hapa hakuna kazi mnayoifanya kelele ni nyingi sana Mwanza serikali inaleta fedha nyingi ilu kukamilisha miradi itakayo wanufaisha wananchi kazi ifanyike kama hauwezi utatupisha tunapokuja kukagua mradi msituuzie mbuzi kwenye gunia kwa kutuonyesha mnafanya kazi kumbe amna mnachofanya tukiondoka na nyie mnaondoka " amesema Aweso.

Pia ameagiza MWAUWASA na RUWASA Mwanza washirikiane kuhakikisha wanakamilisha mradi wa Igongwe na Kahama kwa wakati ili wananchi wapate maji ,pia kwa washauri wote wa miradi amewataka kuacha maigizo bali wafanye kazi kwa bidii na kukamilisha miradi yote kwa wakati na watakaposhindwa kujipanga watasaidiwa.

Amesema adhima ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi wanapata maji safi na salama hiyo ndio Kiu yake hivyo wakandarasi wote watambue hakuna muda wa nyongeza waache janjajanja bali wachape kazi. Naye Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa MWAUWASA  Mhandisi Leonard Msenyele amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi  Oktoba mwaka huu huku kazi zilizopangwa kufanyika zikiwa ni kulanza bomba la Plastiki na chuma kutoka kituo cha kusukuma maji Kiseke hadi tangi la Buswelu kilomita 9.51 ambapo wananchi zaidi ya 100,000 watanufaika .

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema wizara itafatilia utekelezaji kwa ukaribu kwani lengo lao kubwa ni miradi ikamilike kwa wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema Mwanza inakabiliwa na changamoto ya maji hiyo inatokana na maendeleo kwenda kwa kasi kubwa.

Habari Kubwa