Aweso aonya mradi wa maji wa bilioni 24 kuhujumiwa 

25Feb 2021
Marco Maduhu
SHINYANGA
Nipashe
Aweso aonya mradi wa maji wa bilioni 24 kuhujumiwa 

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amewaonya wananchi wa  Mji wa Tinde wilayani Shinyanga pamoja na Mji wa Shelui wilayani Ilamba mkoani Singida, kutohujumu ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria, ambao utatekelezwa kwenye miji hiyo kwa gharama ya Sh. Bilioni 24.4.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Aweso, ametoa onyo hilo leo  Tinde, wakati wa utiaji saini wa mkataba wa ujenzi huo wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria utakaopelekwa kwenye miji ya Tinde na Shelui, ambao ulisainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Athony Sanga na Mkandarasi ambaye ataujenga mradi huo Morali Mohani, kutoka kampuni ya Megha Engeneering Constraction ya nchini India.

Amesema fedha ambazo zinatekeleza mradi huo ni nyingi, na kuwaomba ushirikiano wananchi wa maeneo ambao unatekelezwa mradi huo, wasihujumu mradi wala kuiba vifaa vya ujenzi, bali wautunze vizuri ili upate kuwatatulia kero ya ukosefu wa maji safi na salama.

“Mradi huu wa maji safi na salama utawasaidia kuondokana na adha ya kutafuta maji salama umbari mrefu, pamoja na kupoteza muda wa kufanya shughuli za kiuchumi hivyo naomba muutunze,”anasema Aweso na kuongeza.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum.

“Huu ni mradi wangu wa kwanza kusainiwa nikiwa Waziri wa Maji, nawaomba Wakandarasi vipo vya kuchezea lakini siyo mradi huu, umalizeni kwa wakati na hakutakuwa na muda wa nyongeza,”.

Pia amewaagiza wakandarasi wakati wa kuutekeleza mradi huo, vijana ambao ni wakazi wa Tinde na Shelui ndio watakao pewa kazi na siyo kutoka maeneo mengine, ili wapate vipato na kuinuka kiuchumi.

Mkuu Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.
Mkuu wa Wilaya ya Ilamba mkoani Singida, Emmanuel Ruhahula.

Aidha amezitaka mamlaka za maji ambazo zitakabidhiwa kuendesha mradi huo pale utakapo kamilika na kusambaza huduma ya maji kwa wananchi, wasitoze bili kubwa za maji, bali wafuate viwango vya bili ambazo zinasimamiwa na mamlaka ya udhibiti ubora wa nishati na maji Ewura.

Habari Kubwa