Aweso awasweka ndani vigogo wa maji Mwanza

25Apr 2021
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe Jumapili
Aweso awasweka ndani vigogo wa maji Mwanza

KIMEWAKA Sengerema; Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani Watendaji watano wa serikali na mwakilishi wa Mkandarasi kutokana na kushindwa kusimamia nakusuasua kwa mradi wa maji wa Nyampande uliopo wilayani humo.

Watu hao ni Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa MWAUWASA Mhandisi Leonard Msenyele, Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Sengerema, Mhandisi Cassian Wittike, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mwanza Mhandisi Immaculate Raphael, Meneja Miradi MWAUWASA, Bogadi Mgwatu, Meneja wa Mamlaka ya Maji Sengerema Mhandisi  Robart Lupoja pamoja na mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi huo , 

" OCD wa hapo yupo wapi naomba ukawapumzishe hawa leo tutakutana nao kesho asubuhi kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa  tutakuwa na kikao ukweli lazima kila mtu abebe msalaba wake hatuwezi kukubali mradi ufike asilimia 98 mradi haufanyi kazi alafu mkanipa taarifa za uongo " ameeleza Aweso

 

Habari Kubwa