Azaki zimetajwa kuwa na mchango mkubwa wa maendeleo ya nchini

23Oct 2021
Marco Maduhu
Dodoma
Nipashe
Azaki zimetajwa kuwa na mchango mkubwa wa maendeleo ya nchini

​​​​​​​MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti Omary Kigua, amesema Asasi za Kiraia nchini zina mchango mkubwa katika mapato ya nchi, ajira na upangaji wa Bajeti.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Omari Kigua, ambaye pia ni Mbunge wa Kilindi mkoani Tnga akiwa katika Banda la HakiRasilimali katika wiki ya asasi za kiraia jijini Dodoma.

Kigua ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi Mkoani Tanga, amesema hayo leo Oktoba 23, 2021 alipotembelea Banda la Taasisi ya HakiRasilimali katika maonyesho ya wiki ya Azaki 2021, ambayo yanafanyika Jijini Dodoma.

Amesema, Serikali inatambua mchango wa Asasi za kiraia hapa nchini, katika kukuza maendeleo ya nchi kwa kutoa ajira kwa vijana, pamoja na kuchangia ukuaji wa pato la taifa, ikiwamo Taasisi ya HakiRasilimali ambayo imejikika kwenye Sekta ya uziduaji wa madini, oli na Gesi.

Spika wa Bunge Job Ndugai akiwa katika banda la Taasisi ya HakiRasilimali ambao wanajihusisha na sekta ya uzinduaji wa madini, oil na gesi, kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Rachel Chagonja.

"Katika nchi yetu tuna changamoto ya upungufu wa ajira, Vijana wanaomaliza Vyuo Vikuu ni wengi, na Serikali haiwezi kuwaajiri wote, lakini wapo ambao wanaajiriwa na asasi hizi za kiraia," amesema Kigua.

Kwa upande wa bajeti, Kigau alisema waajiriwa wa asasi hizo wamekuwa wakilipa kodi kama Paye, VAT na Withholding.

Kauli Mbiu ya wiki ya asasi za kiraia kwa mwaka huu 2021 inasema AZAKI kwa maendeleo ya nchi.

Habari Kubwa