Baba aua mwanawe kwa panga

11Jul 2021
Gurian Adolf
Sumbawanga
Nipashe
Baba aua mwanawe kwa panga

JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamsaka, Allon Simfukwe, mkazi wa Kitongoji cha Kaloleni Manispaa ya Sumbawanga kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Kadius Allon (3), kwa kumkata na panga.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, William Mwampaghale, amesema mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuua mtoto wake kwa kumpiga na panga, kwamba tukio hilo lilitokea Julai mosi, mwaka huu katika Kitongoji cha Kaloleni.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta ili achukuliwe hatua za kisheria.

Inaelezwa kwamba licha ya kudaiwa kutekeleza tukio hilo, Simfukwe amekuwa akitoa lugha za vitisho kwa Mwenyekiti wa Mtaa.

Inadaiwa kuwa kabla ya Simfukwe kufanya mauaji hayo alikuwa na mgogoro wa kifamilia na mkewe uliosababisha mwanamke huyo kukimbilia nyumbani kwao na kumuacha mtoto huyo akiwa na baba yake.

Habari Kubwa