Banki ya Dunia yatoa mkopo wa zaidi ya trilioni 2 kwa Tanzania

06Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe Jumapili
Banki ya Dunia yatoa mkopo wa zaidi ya trilioni 2 kwa Tanzania

BODI ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia (WB), imeidhinisha mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni 2 kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi minne ya maendeleo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema hayo leo Juni 6, 2021 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari siku moja kabla ya kuwasilisha bajeti ya Wizara yake ya mwka wa fedha 2021/2022.

Dk Nchemba amesema miradi iliyopata idhini ya bodi hiyo ni mradi wa RISE wenye lengo la kuboresha barabara za vijijini ambao umepewa mkopo wa dola za Marekani milioni 300, mradi wa kusaidia mazingira wa HEET wenye mkopo wa dola milioni 425.

Miradi mingine ni mradi wa DTP wa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao ambao umepewa mkopo wa dola milioni 150 na mradi wa ZESTA wa umeme Visiwani Zanzibar wenye mkopo wa dola milioni 142.

Habari Kubwa