Baraza la madiwani Masasi lapitisha bajeti ya Sh. bilioni 44.3

25Feb 2021
Hamisi Nasiri
Masasi
Nipashe
Baraza la madiwani Masasi lapitisha bajeti ya Sh. bilioni 44.3

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mkoani Mtwara, limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 yenye makisio ya thamani ya Sh. bilioni 44.3.

Mpango huo umepitishwa leo Februari, 25, 2021 wilayani Masasi na Madiwani wa Halmashauri hiyo.

Akisoma mpango huo mbele madiwani hao, makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, ambaye pia ni diwani wa Msikisi, Anthony Chihako, amesema katika rasimu hiyo fedha za miradi ya maendeleo ni 11,898,954,000,00 na fedha za mapato ya ndani ya halmashauri ni 3,538,673,000,00

Amesema utekelezaji wa bajeti hiyo, unategemea ukusanyanyi wa mapato kwa wingi hasa mapato ya ndani na kwa kufanya hivyo hata malengo ya bajeti kupitia miradi iliyopingwa itatekelezeka kwa kama ilivyopangwa.

“Naomba suala la ukusanyaji wa mapato liwe kipaumbele na kutiliwa mkazo halmashauri yetu siyo masikini,tunahitaji usimamizi bora kwenye jambo hili la mapato kwani mapato ya ndani ndio uhai wa halmashauri yetu," amesema Chihako.

Aidha, hoja za baadhi ya madiwani zilijitokeza ni pamoja na kuitaka halmashauri hiyo kuendelea kuongeza vyanzo vipya vya mapato ikiwemo kujenga maghala ya kuhifadhia mazao, kujenga stendi mpya katika kijiji cha Mbuyuni ambako ndiko iliko halmashauri kwa sasa hatua ambayo itasaidia upatikanaji wa mapato ya ndani zaidi.

Habari Kubwa