Bavicha yawajia juu wanaodai kunyanyaswa kingono Chadema

26May 2020
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
Bavicha yawajia juu wanaodai kunyanyaswa kingono Chadema

BARAZA la Vijana la Chadema, Bavicha limedai kushangazwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono zilizotolewa na wabunge wawili wa viti maalum waliohamia katika chama cha NCCR-Mageuzi hivi karibuni.

Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA, Moza Ally.

Akizungumza na The Guardian Digital, Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo bara, Moza Ally amesema malalamiko hayo yaliyotolewa juzi katika vyombo vya habari hayajawahi kutolewa popote katika idara za chama hicho na kudai kuwa yamelenga kukichafua chama hicho.

“Ndiyo mara ya kwanza tumesikia watu wazima wenye watoto wakisema kuwa wamenyanyaswa kingono mnapaswa kujiuliza hawa watu wamekaa bungeni kwa takribani miaka 5 sasa” Moza amesema

 “Hajawahi kusema huko nyuma waje kusema sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi kwetu sisi hiyo ni nia ovu ya kukichafua chama” amesema

Ijumaa iliyopita wabunge wawili wa viti maalum Suzanne Masele na Joyce Sokombi kutoka katika chama hicho walitangaza kukihama chama hicho pamoja na mambo mengine walitaja suala la unyanyasaji wa kingono kama mojawapo ya sababu iliyowatoa Chadema.

Habari Kubwa