Bawacha wamuomba Rais Samia kutolea tamko suala la wabunge 19

21Apr 2021
Enock Charles
Dodoma
Nipashe
Bawacha wamuomba Rais Samia kutolea tamko suala la wabunge 19

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais Samia Suluhu kulihutubia bunge tangu aingie madarakani hapo kesho Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) limemuomba kulitolea tamko suala la wabunge 19 waliofukuzwa uanachama wa chama hicho ambao bado wanahudhuria bungeni.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo Mweka Hazina wa
baraza hilo Catherine Ruge amesema kitendo cha wabunge hao kuendelea
kuhudhuria vikao vya bunge pamoja na kuvuliwa uanachama wa chama
hicho ni kinyume cha sheria.

“Baraza la Wanawake Chadema tunamuomba mheshimiwa Rais Samia akiwa
anaenda kulihutubia  bunge atambue kuna wabunge 19 waliopo bungeni
kinyume cha Katiba na tunamuomba azungumzie jambo hili”
amesema Catherine.

Wabunge hao 19 ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo
Halima Mdee, Katibu Grace Tendega ,aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema
Kanda ya Serengeti Ester Matiko, Ester Bulaya, Nusrat Hanje,Hawa
Mwaifunga na wengineo.

Habari Kubwa