Binti wa kidato cha nne amuua mama yake kisha kumn’goa macho

07Jul 2021
Na Mwandishi Wetu
Kilimanjaro
Nipashe
Binti wa kidato cha nne amuua mama yake kisha kumn’goa macho

MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kindi wilayani ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kumuua mama yake mzazi, Marietha Mushi (62) kwa kumnyonga na shuka, kisha kumpiga na kitu kizito kichwani na kumng’oa macho.

Taarifa imeelezwa kuwa mama huyo alikuwa na ulemavu wa mkono jambo linaelezwa kuwa limechangia ashindwe kujitetea wakati akishambuliwa na binti yake huyo.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Said Mtanda, amesema tukio hilo limetokea Julai 5, 2021 katika eneo la Kibosho Sambarai.

"Mtoto amemuua mama yake na mtoa taarifa ambaye ni kaka wa marehemu ameeleza kuwa alibaini kuuawa kwa dada yake kwa kunyongwa na shuka kisha kupigwa na kitu kizito kwenye paji la uso. Alisema aling’olewa macho na huyu mwanaye wa kike ambaye anasoma kidato cha nne,” amesema Mtanda.

Hata hivyo, mwanafunzi huyo amekamatwa na uchunguzi wa awali wa polisi wamebaini kuwa binti huyo ana upungufu wa akili, na kwa sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi

Habari Kubwa