Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria lazindua mpango wa matumizi maji

25Apr 2021
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe Jumapili
Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria lazindua mpango wa matumizi maji

BODI ya Maji Bonde la Ziwa Victoria imekuwa ya  kwanza kati ya mabonde tisa nchini kuzindua mpango wa matumizi maji katika Bonde la Mto Mara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba alisema Bonde la Mto Mara lina umuhimu wa kipekee katika kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa taifa hasa likigusa nyanja ya ufugaji,uvuvi ,uchimbaji wa madini ,kilimo na utalii pia uchangia maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii sambamba na uhifadhi wa uoto wa asili.

Mhandisi Kemikimba akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga, alisema japo kuwa bonde ilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ya usimamizi wa rasilimali za maji ikiwemo migogoro ya matumizi ya maji hali inayosababishwa na uvamizi na uchafuzi wa vyanzo vya maji ,ongezeko la watu , mifugo,mabadiliko ya tabia nchi hivyo bonde la ziwa kwa kushirikiana na Sustainable Water Partnership (SWP) na World Wide Fund for Nature (WWF) wameandaa mpango wa usimamizi wa matumizi ya maji.

" Mpango huu unalenga kusimamia matumizi ya maji katika bonde la mto Mara na utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji namba 11 ya mwaka 2009 na utasaidia kuwa na matumizi sahihi yenye tija na endelevu ya rasilimali maji , kusaidia viumbe hai vilivyoko ndani ya  mto huo,kilimo,madini na kuendeleza sekta muhimu za uchumi ikiwa pamoja na utalii" alisema Mhandisi Kemikimba.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Dk.Bonaventure Baya, alisema mpango huo utatumika kuoanisha na kuunganisha mpango mkuu wa Bonde la Mto Mara utakaojumuisha nchi mbili Tanzania na Kenya  ambao hapo baadaye watakuwa na mpango mmoja wa maji shirikishi pia mpango huo utapunguza umaskini na kuendeleza riziki kwa wakazi wote kwa kutumia maji ,kutatua migogoro ya watumiaji maji na kudhibiti matumizi ya rasilimali za maji ndani ya bonde hilo. 

Habari Kubwa