Bonite yazawadia pikipiki washindi 45

08Nov 2019
Mary Geofrey
Dar es Salaam
Nipashe
Bonite yazawadia pikipiki washindi 45

KAMPUNI ya Bonite Bottlers Ltd (BBL) ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, jana imewazawadia washindi wake 45 waliojishindia pikipiki, televisheni na katoni za maji ya Kilimanjaro.

Kampuni hiyo inayozalisha vinywaji baridi yakiwamo maji ya Kilimanjaro ilichezesha droo kwanza kwa wateja wake wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.

Katika droo hiyo iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam, jumla ya wateja 15 walishinda pikipiki kila mmoja, 15 televisheni kila mmoja na 15 wengine walishinda kila mmoja katoni 50 za maji.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, muda mfupi kabla ya kuchezeshwa kwa droo hiyo, Meneja Mauzo na Masoko wa Bonite Bottlers Ltd (BBL), Christopher Loiruk, alisema, shindano hilo lilizinduliwa Oktoba 7, mwaka huu na lengo ni kuwashukuru wateja wao kwa kuendelea kutumia maji ya Kilimanjaro.

Aliema droo hiyo ya kwanza kufanyika, imehusisha kanda tano katika mikoa hiyo mitatu kulingana na mgawanyo walioweka ili shindano hilo liwanufaishe wakazi wote wa mikoa hiyo.

Alisema Kanda A inahusisha maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam, Kariakoo, Upanga na Kigamboni; Kanda B inahusisha maeneo ya Tabata, Ilala, Mbagala, Kurasini na Mkuranga wilayani Kisarawe.

Loiruk alisema Kanda C inahusisha maeneo ya Sinza, Mwenge, Kinondoni na Tegeta, Kanda D ni maeneo ya Mbezi Beach, Mikocheni, Masaki na Kibaha na Kanda E inahusisha maeneo ya Manzese, Kimara, Makumbusho, Bagamoyo na mkoa wa Morogoro.

"Lengo la kugawa kwa kanda ni ili wateja wetu wote wanaonunua maji ya Kilimanjaro wanufaike na droo hii na kujishindia pikipiki mpya, televisheni mpya za nchi 32 na maji katoni 50 kila mmoja," alisema Loiruk.

Alieleza zaidi kuwa, lengo ni kuwapata washindi 90 wakiwamo wa watakaoshinda pikipiki 30, televisheni 30 na katoni za maji 150 kwa washindi 30.

Alisema vigezo vya kushiriki shindano hilo ni kwa kila mteja anayenunua maji kuanzia katoni 10 anapatiwa tiketi ya kushiriki droo hiyo na zinashindanishwa kwa kanda ili kuwanufaisha wateja wa maeneo yote.

Loiruk aliwataja washindi 15 wa pikipiki na maeneo wanakotoka katika mabano kuwa ni Isdory Asenga (Kibaha), Manford (Kariakoo), Zubeda Mpili (Mbagala), Ayoub Moukiwa (Uwanja wa Taifa), Gasper Urassa (Palestina), Omega Bupamba (Boko), Mary Goodluck (Dar es Salaam), Debora Njau (Kunduchi), Michael Tesha (Kinyerezi), Godlizen Sam (Masaki), Mary Shokole (Bagamoyo), Alex Mrina (Manzese), Misriya Asnee (Juwata), Sophia Omary na Juma Mbanga (Morogoro).

Washindi wengine 15 wa televisheni kuwa ni Flora Shirima (Agrey), Gabriel Kavina (Banana), Johari Mussa (Tabata), Mary Kimaro (Ilala), Geofrey (Mwananyamala), Erasmos Mwacha (Tegeta), Innocent Adelin (Sinza), Nabel Abdallah (Sinza), Yona Mwanja (Kibaha), Tarimo (Mikocheni), Suzani (Manzese), Mary Joseph (Manzese), Mary Munishi (Morogoro), Antony Chami (Soko), Varelian Mallya (Morogoro).

Washindi wengi 15 walioshinda katoni 15 za maji ni Kenan (Ungindoni), Agnes Massawe (Tabata), Erick Mroso (Kariakoo), Stellah Sanga (Tabata), Godfrey Sebastian (Sinza), Agnes Pascal (Tegeta), Praxeda Paschael (Kinyerezi), Tedi Jeimwami (Kawe), Francis Marandu(Msasani), Jason (Shekilango), Mussa omiro (Kijitonyama), Neema Roita (Mzumbe), Sera Mkasholika (Kingo), Haridy Naganga (Kihonda) na Cornelus (Msasani).

Alisema baadhi ya washindi walipigiwa simu wakati wa kuchezesha droo na wote watapigiwa na kupangiwa siku ya kukabidhiwa zawadi zao zote.

Habari Kubwa