BRELA yashiriki maonesho ya sita ya bidhaa za viwanda vya Tanzania

06Dec 2021
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
BRELA yashiriki maonesho ya sita ya bidhaa za viwanda vya Tanzania

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeshiriki maonesho ya sita ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yaliofanyika leo katika Uwanja wa Maisara visiwani Zanzibar.

Baraka Mwakyalika, kushoto akikabidhiwa Cheti cha Usajili kutoka Afisa wa BRELA kwenye Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.

Ushiriki wa BRELA katika maonesho hayo ni mahususi kulingana na majukumu yake kisheria ambapo imetumia fursa ya maonesho hayo kuhamasisha wamiliki wa viwanda kusajili alama za biashara zao na huduma ili kulinda umiliki wa alama zao.

Pia BRELA imelenga kuwahamasisha wafanyabiashara  kurasimisha biashara zao ili wajulikane katika sekta.

Picha Juu, chini ni Mwekezaji nchini Tanzania,Davide Firno, akipata elimu na usaidizi wa sajili kutoka BRELA kwenye Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania  yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.

Issa Ally Njoka, Mzalishaji wa bidhaa ya Lishe akipata elimu ya alama ya biashara juu ya bidhaa anayozalisha kutoka kwa Afisa Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Haki Miliki, Raphael Mtalima. BRELA inashiriki Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania  yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.
Baraka Mwakyalika, kushoto akikabidhiwa Cheti cha Usajili kutoka Afisa wa BRELA kwenye Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania  yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.
Picha Juu, chini ni Gaston Canuty akipata usaidizi wa karibu wa namna ya kufanya mabadiliko ya taarifa ya kampuni kutoka kwa Afisa kutoka Brela, Paul Peter.  BRELA inashiriki Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania  yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara. 

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Zanzibar wakipata elimu ya namna BRELA inavyotekeleza majukumu yake walipotembelea banda la BRELA kwenye Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.

Habari Kubwa