Bunge kuanza kesho,idadi ya wabunge kupungua kisa corona

30Mar 2020
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Bunge kuanza kesho,idadi ya wabunge kupungua kisa corona

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Bunge litaanza kesho vikao vyake hadi Juni 30, mwaka huu huku akisema idadi ya wabunge watakaoingia ukumbi wa bunge kwa wakati mmoja imepunguzwa kutokana na tishio la corona.

Spika wa Bunge Job Ndugai.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Ndugai amesema muda wa kukutana utapunguzwa kutoka.Amesema vikao vya bunge vitaanza saa nane mchana hadi saa 12 isipokuwa kesho.

"Wabunge watakaoingia kwa wakati mmoja ni 150 kati ya 393, hakutakuwa na maswali kama ilivyozoeleka bali yatafanyika kwa njia ya mtandao na hakutakuwa pia na maswali kwa Waziri Mkuu kabisa kwa Bunge zima,"amesema Ndugai

Spika huyo amesema kuhusu kuwahoji wabunge kuafiki hoja zimeandaliwa kumbi mbalimbali ambazo wabunge watafuatilia kupitia video conference na kuchangia hoja.

"Tutapata orodha ya wabunge ambao wataafiki hoja kwa kuchukua jina na uamuzi aliofanya, siku ya Bajeti ya serikali wataingia wabunge wachache na kutoa kupiga kura na taratibu zingine tutatoa baadae,"amesema.

Kuhusu wageni, Spika huyo amesema wageni wote wasio muhimu wamezuiliwa na hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo kuwekwa vitakasa mikono.

"Kwa kawaida kuna wabunge 393, watumishi wa bunge na watu wengine kulikuwa takribani 700 wanaingia ndani kwa wakati mmoja, tumepunguza idadi ya watu hata kwenu waandishi wa habari,"amesema.

Habari Kubwa