CAG abaini ubadhirifu wa Bil. 34.4/- wizara ya maliasili na utalii

08Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
CAG abaini ubadhirifu wa Bil. 34.4/- wizara ya maliasili na utalii

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amebaini ubadhirifu wa Bil. 34.3/- katika Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zilitolewa kinyume na taratibu za nje ya bajeti.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Ddoma leo Aprili 8, 2021Kichere amesema kuwa mkurugenzi wa utalii wakishirikiana na mhasibu walitumia vibaya tozo za utalii.

“Waziri wa Maliasili na Utalii kupitia kaimu katibu wake aliagiza Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Wakala wa Misitu (TFS) kugharamia matumizi ya Waziri jumla ya Sh. Milioni 118.4 kinyume na taratibu na nje ya bajeti ya taasisi hizo,”

“Katibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliagizaNgorongoro na TANAPA kulipa Shilingi 172 Milioni kugharamia Kill Challenge la kuhamasisha wasanii kupanda Mlima Kilimanjaro nje ya bajeti ya taasisi hizo na hakukuwa na risiti za malipo,’’

"Mkurugenzi wa utalii na mhasibu walitumia vibaya fedha za tozo ya utalii jumla ya Bilioni 34.3,” amesema Kichere.

Habari Kubwa