CCM kushughulikia viongozi wanaopotosha umma

26Jul 2021
Beatrice Shayo
Dar es Salaam
Nipashe
CCM kushughulikia viongozi wanaopotosha umma

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, amesema hatua kali zitachukukiwa kwa baadhi ya viongozi wao ambao wamekuwa wakipotosha umma.

Shaka amesema CCM inafuatilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa chama na Rais Samia Suluhu Hassan.

"CCM inawakikishia wanachama na watanzania kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi iyo kusukuma ajenda zao binafsi, kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM," amesema Shaka.