CCM kuzindua kampeni za ubunge Ushetu

26Sep 2021
Na Mwandishi Wetu
Shinyanga
Nipashe Jumapili
CCM kuzindua kampeni za ubunge Ushetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM),  kimezindua kampeni za Ubunge katika Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga.

Kampeni hizo zitazinduliwa na Naibu Katibu Mkuu wa  CCM Tanzania Bara Christina Mndeme.

Mndeme, atatumia fursa hiyo kuhutubia wananchi wa Ushetu, kunadi Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya 2020 hadi 2025 na kumuombea kura mgombea wake Emmanuel Cherehani.

Maandalizi ya ufunguzi wa kampeni hizo yanaendelea, katika viwanja  vya Nyamilangano vilivyopo Wilayani Kahama.

Hatua ya uchaguzi huo imefikiwa baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ushetu ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi Ellas Kwandika kufariki dunia.

Kwandika alifariki dunia Agosti 2, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kuzikwa Agost 9 mwaka huu, Ushetu mkoni Shinyanga.

Habari Kubwa