CCM: Tutayapata majimbo upinzani kwa gharama yoyote

07Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
CCM: Tutayapata majimbo upinzani kwa gharama yoyote

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Abdallah Burembo amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakitakubali kuyakosa tena majimbo ya Mkoa wa Kigoma yanayoongozwa na upinzani, kwamba watayapata kwa gharama yoyote katika uchaguzi ujao

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Abdallah Burembo

Burembo ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Kigoma ametoa kauli hiyo wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa mkoa wa Kigoma wa kumchagua mwenyekiti wa mkoa huo, na kuwataka viongozi wa chama hicho mkoa wa Kigoma kuwafichua watendaji na wakurugenzi ambao hawafuati utekelezaji wa ilani ili watolewe.

"Serikali ni ya Chama cha Mapinduzi, waliopo chini ya serikali wanaitumikia serikali na kutekeleza ilani yetu, kama kuna watendaji au mkurugenzi hafuati utekelezaji wa ilani tutawatoa, hatuwezi kukubari tuyakose majimbo haya, tunayataka kwa gharama yoyote ile," alisema Burembo.

Mojawapo ya majimbo mkoani Kigoma yanayoongozwa na upinzani ni Jimbo la Kigoma mjini linaloshikiliwa na Chama cha ACT-Wazalendo, ambalo mbunge wake ni Zitto Kabwe.

Habari Kubwa