CCM wilayani Siha watakiwa kugombea nafasi ndani ya chama

20Jan 2022
Anjela Mhando
SIHA
Nipashe
CCM wilayani Siha watakiwa kugombea nafasi ndani ya chama

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wametakiwa kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali za uongozi zinazopatikana ndani ya chama hicho ikiwemo nafasi za uongozi pamoja na nafasi za Jumuiya ya CCM.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa CCM wilayani, Ally Kidunda katika ziara ya Sekretarieti ya CCM ailiyofanyika katika Kata za Gararagua, Karansi Mitimirefu Sanya Juu , Ndumenti, Ngarenairobi.

Kidunda amesema mwaka huu watafanya uchaguzi wa Jumuiya za CCM ambapo inapangwa safu kuelekea 2024/25.

Amesema kuwa itakuwa ni jambo la kusikitisha kama wanaCCM watawapa nafasi za uongozi watu ambao sio wanachama bali ni wavaa nguo za CCM lakini kwenye mioyo yao sio wa chama hicho.

Amewakumbusha wanachama wa CCM kuwa mabadiliko ya kisiasa  ndani yanakuwaga na hila kwani kuna wanasiasa wengine wanatamani kuingia ndani ya chama hicho na kumbe ni maluki.

"Muda utafika tuangalie watakao chukua fomu, kama ni wenzetu kweli wanachukua nafasi hizo kwa nia ya dhati  kutumikia chama au wanakuja  kutumika, tushughulike nao  tusiwape nafasi ndani ya chama chetu," amesema.

Habari Kubwa