CCM yampitisha Mwinyi mgombea Urais Zanzibar

10Jul 2020
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
CCM yampitisha Mwinyi mgombea Urais Zanzibar

HALMASHAURI KUU ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imempitisha Dk.Hussein Mwinyi  kuwa mgombea Urais wa Chama hicho Zanzibar  katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwa kura 129 sawa na asilimia 78.65.

Dk.Hussein Mwinyi.

Katika matokeo ya uchaguzi wa ndani wa chama hicho yaliyotangazwa na Spika wa bunge, Job Ndugai ,Dkt Hussein Mwinyi ameshinda uchaguzi huo akifuatiwa na Khalid Mohammed aliyepata kura 11.58 sawa na kura 19 huku Shamsi Nahodha akiambulia kura 16 sawa na asilimia 9.75.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi  mgombea huyo wa chama cha mapinduzi amewaomba wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo kuendelea kumpa ushirikiano ili kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi.

“Leo tumemaliza namshukuru Mwenyezi Mungu huku nikijua kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa zaidi asanteni sana wote walionipigia kura za ndio nashukuru na wale ambao wamewapigia wengine nawashukuru kwa kutumia haki yao ya Kikatiba” amesema Mwinyi

Uchaguzi  Mkuu wa kuchagua viongozi kwa nafasi ya Urais ,Ubunge na Udiwani unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu na tayari vyama vimeshaanza michakato ya ndani kuandaa wagombea wao.

Habari Kubwa