CCM yarudisha jimbo la Arusha Mjini mikononi mwake

29Oct 2020
Na Mwandishi Wetu
Arusha
Nipashe
CCM yarudisha jimbo la Arusha Mjini mikononi mwake
  • Baada ya miaka kumi ya kuwa kwenye mikono ya upinzani, sasa, CCM imeweza kushinda ubunge jimbo la Arusha .

Aliekuwa Mkuu wa Mkoa Arusha, Mashaka Mrisho Gambo wa CCM amechaguliwa kuwa Mbunge mpya wa Arusha Mjini akiwa amepata zaidi ya kura 80,000.

Aliekuwa Mkuu wa Mkoa Arusha, Mashaka Mrisho Gambo wa CCM amechaguliwa kuwa Mbunge mpya wa Arusha Mjini akiwa amepata zaidi ya kura 80,000.

Huu ni ushindi mwingine mkubwa kwa CCM ambayo sasa imeweza kurudisha Arusha Mjini kutoka kambi ya upinzani ambayo ilishikilia jimbo hilo kama ngome kuu kwa miaka kumi sasa.

Mbunge mteule Gambo amemshinda mbunge mtetezi Godbless Lema kutoka chama cha upinzani cha Chadema.

CCM pia imepata ushindi mkubwa Same Mashariki na Magharibi ikiwa Mama Kilango Malecelaameshinda ubunge Same Mashariki na Dkt. Mathayo David akitwaa ushindi Same Magharibi.

Matokeo ya uchaguzi wa Tanzania Bara bado yanaendelea kutangazwa, usipitwe endelea kutufuatilia: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa