CCM yatamba kushinda Zanzibar na Bara

08Feb 2020
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
CCM yatamba kushinda Zanzibar na Bara

MAKAMU Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi , Abdallah Hajj Haider amesema Chama na serikali zake katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu zitarudi kama zilivyo hivi sasa na wale wanaobeza kuhusu Zanzibar hawajui ukweli.

MAKAMU Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi , Abdallah Hajj Haider.

Haider ametoa kauli hiyo leo katika kongamano la maadhimisho ya miaka 43 ya kuzaliwa kwa CCM mkoani Dodoma.

Amesema “CCM na serikali zake zitarudi kama ilivyo sasa sisi ndio tunaoitambua Zanzibar msishtuke na hizi kelele za mlango uchaguzi sisi tumeshamaliza wakitaka wasitake, uchaguzi lazima na tutashinda lazima hii ndio kauli ya CCM na kauli ya wazazi, kwamba serikali mbili za Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania na Zanzibar zitabakia milele na milele.”

Soma zaidihttps://bit.ly/379xUsD

aye,  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye ni mlezi wa mkoa wa Dodoma Leyla Ngozi amewataka wanachama kuiga utumishi uliotukuka wa mzee Mangula ambaye tangu awe mtumishi wa Chama mpaka sasa hakuna makando kando yake yoyote yaliyosikika.

“Mzee Mangula ni mfano wa kuigwa ,tangu utumishi wake mpaka leo hatujawahi kusikia tuhuma zake zozote,hana makando makando,viongozi wote mliopo hapa tutakaposikiliza maelezo yake tuyapokee lakini kila mtu atoke akiwa na hamasa ya kumuuiga,”amesema Mlezi huyo.

Amesema CCM imejipanga vyema katika mkoa huo na wapinzani hawana nafasi yoyote kwak uwa hawataruhusu jimbo lolote la mkoa huo liende upinzani.

Akitoa salamu za serikali Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amesema idadi ya watu waliohudhuria imedhihirisha utendaji mzuri wa chama hicho katika ahadi zake ilizoziweka kwenye Ilani ya Uchaguzi ikiwemo kuhamishia serikali Dodoma.

“Pongezi kwa CCM,miaka 43 sio kidogo ni mingi sana,ndani ya nchi tunashuhudia amani,umoja na mshikamano uliosimamiwa na chama hiki,mahala pengine duniani wameshindwa kudumisha haya lakini hapa kwetu Tanzania imewezekana chini ya CCM,hongereni sana,”amesema Dk. Mahenge.

Amesema yote mazuri yamewezekana kwa sababu CCM ni chama cha watu na sio chama cha mtu binafsi kama ilivyo kwa vyama vingine vya siasa.

Akitoa maelezo kuhusu maadhimisho hayo Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph amesema Kamati ya siasa ilifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea na kukagua miradi 30 katika halmashauri nane zilizopo katika mkoa huo.

“Pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani pia tumewafariji waliopatwa na mafuriko katika wilaya za Bahi,Chemba na Kondoa,tumewatembelea wagonjwa na wenye mahitaji maalum ,tumekarabati ofisi za chama ,tumefanya harambee iliyolenga kupata fedha za kukamilisha jengo la chama na kitega uchumi cha kata ya kilimani,tumepanda miti na kufanya usafi pia,”ameongeza Jamila.

Habari Kubwa