CCM yazindua kituo taarifa za rushwa za uchaguzi

02Jun 2020
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
CCM yazindua kituo taarifa za rushwa za uchaguzi

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeanzisha kituo cha taarifa za uchaguzi kitakachotumika kuripoti matukio ya rushwa za uchaguzi zinazotokea katika chama hicho ambayo yatatumwa kwa kutumia namba maalumu ya WhatsApp iliyotolewa na chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Akizungumza katika vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  kuwakamata  watakaobainika kutoa rushwa ili kuchaguliwa.

“Ukiona mtu anatoa rushwa wewe unachofanya mrekodi tu kimyakimya akisema ooh unajua mimi naleta maji sijui barabara ni muongo mkubwa wewe unaleta maji wapi? serikali inafanya hivyo,” amesema Polepole

Amesema hakuna mwanachama yeyote wa chama hicho aliyeagizwa kuchangisha fedha kwa ajili ya mgombea urais wa chama hicho au kuagizwa na mojawapo ya viongozi wa chama hicho kugombea jimbo fulani na kwamba wanaosema hivyo ni matapeli wa kisiasa.

Kauli hii ya Polepole imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Takukuru Mkoa wa Kinondoni kuwakamata makada sita wa chama hicho kwa madai ya rushwa maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam jana.

Habari Kubwa