Chadema yatoa majina ya wagombea Ubunge awamu ya kwanza

09Aug 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Chadema yatoa majina ya wagombea Ubunge awamu ya kwanza

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemteua Asia Msangi kuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga, John Mrema kugombea Jimbo la Segerea, Halima Mdee Jimbo Kawe,Jimbo la Ubungo ni Boniface Jacob, Bagamoyo Emmanuel Lukumay, Kibaha Edward Kinabo, Kibiti Kulwa Lubuva, Mafia Omary Hassan.

wanachama wa chadema wakiwa katika moja ya mikutano yao. picha ya mtandao.

Orodha hiyo ya majina ya awamu ya kwanza imetolewa leo Agosti 9, 2020, na kuhusisha majimbo 163 kutoka katika kanda 8, ambazo ni kanda ya Kati, Kanda ya Nyasa, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Serengeti, Kanda ya Viktoria, Kanda ya Kusini, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Pwani.

Majina mengine yaliyochaguliwa kuwania ni pamoja na John Heche, wa jimbo la Tarime Vijijini, Ester Matiko Jimbo la Tarime Mjini, Ester Bulaya jimbo la Bunda Mjini, Godbless Lema jimbo la Arusha Mjini, Rebecca Mgondo Arumeru Mashariki, Jimbo la Siha ni Elvis Mos, Moshi Vijijini Lucy Ndesamburo, Rombo ni Patrick Assenga.

 

Habari Kubwa