Chadema yamjibu IGP, Polisi kutumia bunduki uchaguzi mkuu

02Jun 2020
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
Chadema yamjibu IGP, Polisi kutumia bunduki uchaguzi mkuu

SIKU moja baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, kusema atahakikisha uchaguzi unafanyika kwa hali ya amani na utulivu na kutoruhusu mtu yeyote kucheza na bunduki kuwatisha Watanzania, Chadema kimemtaka mkuu huyo kuagiza polisi kutokuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Akiongea na The Guardian Digital, Mkuu wa Idara ya habari ya chama hicho, Tumaini Makene amesema kuwa uchaguzi sio tukio la siku moja na kwamba vyama vya siasa vina wajibu wa kujiandaa na uchaguzi huo ikiwemo kufanya mikutano ya ndani nay a hadhara.

“Tunataka IGP atoe kauli madhubuti  kwa ajili ya imani na matumaini ya amani na utulivu kwamba jeshi la polisi litasimamia haki katika uchaguzi huo na kutoa maelekezo thabiti kwa wadau wote wakiwemo ma RPC na maOCD” amesema Makene

Akizungumza kwa nyakati tofauti na Askari Polisi wa mikoa ya Tabora na Singida hivi karibuni mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini alisema jeshi la polisi lina wajibu mkubwa kwenye uchaguzi mkuu na kuwataka askari kutoruhusu mtu yeyote kutocheza na bunduki kuwatisha Watanzania.

 

SOMA ZAIDI-https://www.ippmedia.com/sw/habari/igp-hatutaruhusu-mtu-kucheza-na-bundu...

Habari Kubwa