Chalamila kutembeza bakora kwa wasiolewa na kuoa

18Oct 2019
Anaeli Mbise
Dar es Salaam
Nipashe
Chalamila kutembeza bakora kwa wasiolewa na kuoa

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kuwa hivi sasa wanatumia bakora katika kila jambo hata kwa watu ambao wanakaa tu nyumbani wakati wamefikisha umri wa kuoa na kuolewa.

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Chalamila amesema kuwa bakora ndiyo njia pekee ambayo inasaidia katika kunyoosha mambo.

"Maana siku hizi tumeanza kutumia viboko kwenye kila jambo hata tukikuta umekaa pale nyumbani uolewi ni bakora tu kwamba nenda katafute mume, tunakuona umekaa pale nyumbani huoi ni bakora tu wewe nenda katafute mke.," amesema Chalamila na kuongeza kuwa

"Kuna umri ambao unatosha lazima uchangamshwe kwa hiyo viboko vinasaidia," amesema 

Hata hivyo katika mitandao ya kijamii kuna video imesambaaa ikimuonyesha Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto Dkt. Getrude Lwakatare, akiwaombea waumini wake wakike na kiume ambao hawajaolewa wala kuoa.

Katika video hiyo, Mchungaji Lwakatare ameita maombi hayo ni ya upepo wa kisulisuli 'upepo wa miujiza' uvume na kuwaleta wanaume katika kanisa hilo kwa ajali ya kuwaoa wanawake ambao wanahitaji wanaume.

 

Habari Kubwa