Chalamila awataka watu kuacha kumsema vibaya Hayati Magufuli

19Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Chunya
Nipashe
Chalamila awataka watu kuacha kumsema vibaya Hayati Magufuli

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amewataka watu kufanya kazi kwa bidii na kujadili mipango ya maendeleo kuliko kupoteza muda kumsema vibaya aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Magufuli.

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Chalamila amesema hayo Leo wakati akiongea na wachimbaji wadogo wa madini wilayani Chunya.

"Wengine nimesikia kwenye mijadala wanasema Rais Magufuli alikuwa dikteta, ukimuona mtu anatokea sasa hivi anaanza kuongea wakati aliyekuwa Rais (Magufuli) amefariki ujue huo ni mjadala hewa, msijiingize kwenye mijadala hiyo”

“Mijadala sahihi itakayotutoa kimaisha ni kazi sio mijadala hewa, kama kuongea jambo lenye maana basi ilifaa mumfikishie ujumbe wakati akiwa hai mkianza kueleza mambo ambayo yeye amefariki mnatuchosha akili”

“Mjadala wa kweli ni kuuliza umeme uko wapi?, mbona Barabara haijatengenezwa?, mbona mawasiliano hakuna?, mjadala wa kweli nikusema hapa kuna watu wanatudai kodi wanatunyanganya kwa nguvu, tupate vituo vya afya vizuri, Shule nzuri, tuwe na maisha bora, mijadala hewa tuipotezee haitatufikisha tunakokwenda” amesema Chalamila.

Habari Kubwa