Chanjo ya corona haina madhara - DC Makalla

29Jul 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Chanjo ya corona haina madhara - DC Makalla

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amewasihi Wananchi kuhakikisha wanapokea chanjo ya corona kwa ajili ya kulinda afya zao.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla.

Makalla akiwa ni miongoni mwa viongozi waliopata chanjo wakati ikizinduliwa jana Julai 28,  amesema kuwa tangu amepokea chanjo hiyo hajapata madhara yoyote kiafya.

Hata hivyo, RC Makalla amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kuonyesha mfano kwa kupata chanjo na kutimiza wajibu wake wa kuwaletea chanjo wananchi wake.

Aidha, RC Makalla ameendelea kuwasisitiza Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Corona huku akisisitiza uvaaji wa barakoa wawapo kwenye vyombo vya usafiri na suala la ‘level seat’.