Chanzo cha Ebola Uganda hiki hapa

12Jun 2019
Zanura Mollel
LONGIDO
Nipashe
Chanzo cha Ebola Uganda hiki hapa

Mkuu wa ldara ya Afya kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dk Charles Katende ameeleza kuwa chanzo cha ugonjwa wa Ebola nchini Uganda ni kutokana na mwingiliano wa wasafiri kati ya raia wa Uganda na Congo.

Mkuu wa ldara ya Afya kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dk Charles Katende.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Dk. Katende ameeleza kuwa familia moja huko nchini Uganda ilisafiri kuelekea Congo kwa ajili ya mazishi na waliporejea nchini Uganda walirudi na mambukizi ya ugonjwa wa Ebola.

"Walienda Congo kumzika baba yao bahati mbaya waliporejea Uganda mtoto wao wa miaka mitano akaanza kuugua na walipompeleka hospitali vipomo vikabainika kuwa amepata maambukizi ya Ebola," amesema Dk. Katende

Amedai kuwa taarifa za kuingia kwa Ebola nchini Uganda zimepatikana jana kupitia Shirika la Afya Duniani (WHO) na vyombo vya afya mbalimbli kutoka nchini humo,lakini hadi sasa hajapokea taarifa ya kifo kutokana na ugonjwa huo.

" Familia hiyo iliyopata maambukizi, ipo chini ya uangalizi huku wakiendelea kupata matibabu pamoja na chanjo " Amedai Dk Katende

Kupitia taarifa iliyoripotiwa na chombo cha Habari nchini Ujerumani (DW) mtoto huyo  amefariki dunia.

Habari Kubwa